Nililetwa kufanya Ukahaba: Wanawake wa Afrika waliopelekwa India kwa ajili ya ngono

Maelezo ya video, Nililetwa kufanya Ukahaba: Wanawake wa Afrika waliopelekwa India kwa ajili ya ngono

BBC Africa Eye imefichua mtandao unawashawishi wanawake wa Kiafrika kwenda India, ambako wanalazimika kufanya ukahaba ili kuwaridhisha wanaume wa Kiafrika wanaoishi New Delhi.

Paspoti zao zinachukuliwa na matembezi yao kudhibitiwa hadi watakapolipia gharama kubwa waliyotumia kusafiri kwenda India.

Nyasha Kadandara anasimulia zaidi.