Nililetwa kufanya Ukahaba: Wanawake wa Afrika waliopelekwa India kwa ajili ya ngono
BBC Africa Eye imefichua mtandao unawashawishi wanawake wa Kiafrika kwenda India, ambako wanalazimika kufanya ukahaba ili kuwaridhisha wananaume wa Kiafrika wanaoishi New Delhi.
Paspoti zao zinachukuliwa na matembezi yao kudhibitiwa hadi wantakapolipia garama kubwa waliyotumia kusafiri kwenda India. Nyasha Kadandara anasimulia zaidi ...
