Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je ni kweli watoto wanaokuwa bila baba huenda wakawa wahalifu
Watoto wanaokuwa bila malezi ya baba au baba mlezi huenda wakajiingiza katika uhalifu baadae maishani. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na idara ya magereza nchini Kenya.
Utafiti huo unasema kuwa 46% ya wafungwa hawana baba au wanatoka katika familia zilizosambaratika. Watafiti wanasema baba wanatakiwa kuhamasishwa athari ya kutokuwa katika maisha ya watoto wao.