Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mafuriko Afrika mashariki: Jinsi mvuvi huyu wa Kenya alivyookolewa na ndege katika mafuriko
Mvuvi mmoja amenusuriwa kutoka kwa kisiwa ambacho alikuwa amekwama tangu siku ya Ijumaa kutokana na mafuriko makali.
Vincent Musila alikuwa amekwenda kuvua samaki kama kawaida katika mto mmoja mjini Thika katikati mwa Kenya wakati mto huo ulivyovunja kingo zake.
Watu wengi walitazama bila usaidizi wowote walipokuwa wakisubiri usaidizi wa dharura ili kumuokoa.