Solomon Serwanjja: Mwandishi wa Uganda ashinda tuzo ya Komla Dumor
Mwandishi mpekuzi na msomaji habari kutoka nchini Uganda, Solomon Serwanjja ameshinda tuzo ya Komla Dumor ya BBC World News 2019. Solomon ni mtangazaji katika televisheni ya NBS TV nchini Uganda ambako anatangaza mojawapo ya vipindi vikuu vya kituo hicho, amewahi pia kutengeneza ripoti zilizoshinda tuzo, ikiwemo makala ya BBC Africa, Africa Eye, yaliomsukuma kwenye mwanga barani Afrika kwa uandishi habari wake mkakamavu.

