Waihiga Mwaura kutoka Kenya ashinda tuzo la BBC la Komla Dumor

Maelezo ya video, Waihiga Mwaura kutoka Kenya ashinda tuzo la BBC la Komla Dumor

Mwandishi wa habari mkenya na mtangazaji wa televisheni ndiye mshindi wa mwaka huu wa tuzo la BBC la Komla Dumor.

Waihiga Mwaura ni msomaji wa habari wa jioni kwenye kituo kinachotazamwa sana Kenya cha Citizen.

Kama sehemu ya tuzo hiyo, kwa miezi mitatu atakuwa kwenye ofisi ya BBC mjini London na baadaye kurudi Afrika kuendelea na kazi.