Kenya: Wakazi wa Turkana walalamikia kutonufaika na mafuta

Maelezo ya video, Kenya: Uchimbaji mafuta .

Kampuni ya Tullow ilipogundua mafuta kusini mwa bonde la Lokichar mwaka 2012, wenyeji walidhani kwamba eneo hilo lililotengwa hatimaye litaanza kustawi.

Inasemekana kwamba bonde hilo lina uwezo wa kutoa mapipa milioni 560 ya mafuta katika vyanzo ilivyo navyo. Lakini miaka saba baadaye, wenyeji bado hawajapata manufaa ya kuridhisha.

Hivi karibuni Rais Kenyatta alizindua shehena ya bareli 240,000 ambayo iliuzwa kwa dola milioni 12.

Wenyeji wa eneo la Lokitoeliwo lililopatikana mafuta, walilitumia kulisha mifugo lakini kwa sasa linatumika kwa uchimbaji wa bidhaa hiyo kwenye visima vya eneo la Ngamia ambalo wanadai kukumbana na ukosefu wa maji, umaskini na njaa.