Bobi Wine: Mpinzani wa rais Museveni katika uchaguzi mkuu Uganda 2021

Maelezo ya video, Bobi Wine: Mpinzani wa rais Museveni katika uchaguzi mkuu Uganda 2021

Bobi Wine ameanza kwa kuwa muimbaji mashuhuri na sasa ni mbunge nchini Uganda anayesema atapambana na rais wa muda mrefu nchini humo Yoweri Museveni katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

Mwanasiasa huo wa miaka 37 anatumai kuwa mgombea wa vijana wa Uganda, walio zaidi ya nusu ya idadi jumla nchini.

Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga amezungumza na mwanamuziki huyo kuhusu mipango yake ya siku za usoni.