Wagonjwa na wahudumu wa Saratani kenya waandamana

Wagonjwa na wahudumu wa ugonjwa wa saratani wameandamana kuishinikiza serikali kuondosha gharama kubwa za matibabu kwa ugonjwa huo nchini.

Saratani
Maelezo ya picha, Waandamanaji wanasema matibabu zikiwemo dawa ni ghali mno kumudu kwa baadhi ya wanaogunduliwa kuwa na ugonjwa huo. Miriam Shikami aligunduliwa kuwa na saratani ya saratani ya shingo ya uzazi mnamo Agosti mwaka jana iliokuwa katika kiwango cha pili. Amepokea huduma ya chemotherapy mara sita na ikabidi asitishe matibabu hayo baada ya kemikali kuyaathiri miguu yake.
Saratani
Maelezo ya picha, Watoto walio hadi chini ya miaka 12 waliopona saratani pia walikuwemo katika maandamano ya leo. Takwimu kutoka wizara ya afya Kenya inaonyesha kuwa visa 47,887 vipya vya saratani huripotiwa na watu 32,987 hufariki kila mwaka.
Saratani
Maelezo ya picha, Jacquezdean Gatehi ana umri wa miaka 13. Anaugua saratani ya mifupa ambayo aligunduliwa mwaka mmoja uliopita. Mamake Elizabeth Nyambura anaeleza walikabiliwa na hali ngumu kutokana na kwamba madakatari hawakumpatia muda wa hata kufikiria saratani nini. Anasema alibwagia taarifa hizo kwa mshindo ambao hatowahi kuusahau. Anasema kwa namna ambavyo aliarifiwa, alihisi hata kujitoa uhai. 'Ilikuwa kama hukmu ya kifo' anasema Nyambura.
Saratani
Maelezo ya picha, Inakadiriwa pia kuna visa 3,200 vipya vya saratani miongoni mwa watoto walio chini ya miaka 18. Saratani 5 zinazodhihirika pakubwa nchini ni ya matiti, shingo ya uzazi, ya koo, saratani katika kibofu cha haja ndogo na ya utumbo.
Saratani
Maelezo ya picha, Joan Wangare aligunduliwa na saratani ya Kongosho mnamo 2011 alifanyiwa upasuaji na kupokea matibabu na kufanyiwa chemoHatahivyo anakumbuka alivyochukuwa muda kabla kutambua nini hasaa kilichokuwa kumsibu. Anasema alikwenda hospitali baada ya kuanza kuwashwa mwili sana na kwa kiasi fulani aliishia kupewa dawa za ugonjwa ambao hanao - alitibiwa kwa mzio. Hivi sasa ana miaka minane tangu augue, na anasema anasikia nafuu. Anatarajiwa kurudi kufanyiwa ukaguzi Oktoba.
Saratani
Maelezo ya picha, Wagonjwa na wauguzi walioandamana wanataka rais nchini atangaze saratani kuwa ni janga la kitaifa. Wanasema iwapo hatua hiyo itaidhinishwa basi rasilmali nyingi zitaelekezwa katika kutoa matibabu ya nafuu na yanayowafikia wote nchini pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalamu na kuweka vifaa hospitalini katika kukabiliana na ugonjwa huo.