Tabisha Esperance: Mbunifu mitindo katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma
Tabisha Esperance alitoroka vita katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mnamo mwaka 2010. Alitengana na familia yake na kuishia katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma kaskazini mashariki mwa Kenya. Kadri miaka ilivyosogea, amefanikiwa kuyabadilisha maisha yake kutokana na kipaji alichonacho cha kubuni mitindo ya mavazi. Amejipatia umaarufu na sasa anaazimia kuwavalisha nyota wa Afrika akiwemo Yemi Alade.
Video: Anne Okumu na Anthony Irungu