Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simba vs Sevilla: Hisia ya mashabiki wa Simba
Mabingwa wa soka Tanzania, Simba SC almanusura iandike Historia kwa kuitandika Sevilla ya Hispania iliyosheheni nyota wake kibao. Katika mchezo wa kirafiki uliovuta hisia za mashabiki wengi Afrika Mashariki, Simba imelala kwenye uwanja wa nyumbani jijini Dar es Salaam kwa kufungwa mabao 5-4 dhidi ya Sevilla.