Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Watoa huduma za kitalii walilia pendekezo la kuidhinishwa magari ya umeme Mlima Kilimanjaro
Umoja wa watoa huduma za kitalii kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wamelipokea kwa hisia tofauti wazo la serikali ya Tanzania la kutaka kuanzisha utalii wa siku kwa kutumia magari ya umeme.
Kwa mujibu wa taarifa za awali njia inayopendekezwa ni ile ya Machame ambayo kwa watoa huduma, ndio njia inayotumika na wageni zaidi kuliko njia nyingine zote kuelekea mlimani.
Eagan Salla akiwa mkoani Kilimangaro alizungumza na wadau mbali mbali: