Je Zitto Kabwe ana mpambanuaje Maalim Seif baada ya kujiunga na ACT Wazalendo Tanzania

Maelezo ya sauti, Je Zitto Kabwe ana mpambanuaje Maalim Seif baada ya kujiunga na ACT Wazalendo Tanzania

Mwanzoni mwa wiki hii Mahakama Kuu ya Tanzania, ilitoa uamuzi wa kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama CUF, hatua iliyomfanya Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, kukihama na kujiunga na Chama cha ACT-WAZALENDO.

Bado wengine wanajiuliza maswali. Mwandishi wa BBC Zuhura Yunus amepata fursa ya kuzungumza na Zitto Kabwe na kutaka kujua ilikuaje mpaka ACT ikaungana na wafuasi wengi wa CUF.