Wakenya wataka serikali kushughulikia tatizo la ukame

Wakazi wa maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Kenya bado wanakabiliwa na baa la njaa wengi wao wanaendelea kuomba msaada wa wahisani kuokoa maisha yao huku zaidi ya wakazi 11 wakiripotiwa kufariki kutokana na ukosefu wa chakula.

Mwanahabari wa BBC Roncliffe Odit amezungumza na Gavana wa Turkana Josphat Nanok kuhusu ukubwa wa baa hilo.

Kumekua na maoni mbalimbali kuhusu hali ilivyo Turkana, baadhi wakiona kuwa kutegemea misaada hakusaidii, isipokua Serikali ifanye jitihada kuwasadia raia kupata njia nzuri ya kukomesha baa kama hilo kujitokeza siku za usoni.