Faru weupe wa kaskazini wanakabiliwa na tisho la kuangamia kabisa duniani

Maelezo ya video, Hatma ya kizazi cha faru weupe wa kaskazini ni ipi?

Taarifa ya kifo cha faru mweupe wa kaskazini aliyefahamika kama Sudan iligonga vichwa vya habari kimataifa hasa pale ilipobainika kuwa faru wa aina hiyo sasa wamebakia wawili pekee duniani.

Sudan alifariki mwezi Machi mwaka 2018 na kuacha pigo kubwa katika juhudi za kuwahifadhi wanyama hao ambao wanakabiliwa na tisho la kuangamia kabisa duniani.

Hatima ya baadae ya faru weupe wa kaskazini imesalia mikononi mwa wanasayansi waliyoanzisha mradi wa kuwazalisha wengine kutokana na mbegu za Sudan zilizohifadhiwa katika maabara.