Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ruth Wacuka Kimani: Mjasiriamali anayejikimu kwa kufuma
Ruth Wacuka Kimani mwenye umri wa miaka 46 kutoka mtaa wa Kahawa mjini Nairobi Kenya, alianza kufuma kama njia ya kujipunguza mawazo baada ya kupoteza kazi yake. Aliugua na kulazimika kutumia akiba yake ya mwisho kwa matibabu, hapo ndipo anasema kipaji chake kilipogeuka kuwa tiba na kipato kwake.
Alianza kwa kiasi cha $5, na sasa imegeuka kuwa biashara inayomkimu maisha. Yeye hufuma akitembea, akisafiri, mchana na hata usiku.
Wengi wanamshangaa, lakini anasema kufuma kwake ni kama dozi ya dawa asiyoweza kuiacha. Ruth huuza bidhaa zake katika mitandao ya kijamii na pia kutokana na kusambaa kwa sifa kutoka kwa wateja wake kuhusu bidhaa zake.
Video: Faith Sudi.