Mfungwa apatikana paruwanja akijaribu kutoroka jela

Mpango wa mfungwa huyu kutoroka jela kijanja uligonga mwamba baada ya dari la chumba alichokuwa amejificha kuporomoka. Raia huyo wa Marekani Blaze Ayers alitoroka alipokuwa akipelekwa kwenye seli yake. Walinzi walimkimbiza lakini alifanikiwa kuingia kwenye sehemu ya dari la chumba hicho. Matokeo yake ikawa ni kuanguka mbele ya walinzi waliokuwa wakimtafuta.