Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Phuti Lekoloane: Mchezaji soka anayebadili mitazamo dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Afrika
Katika mataifa mengi Afrika, ni uhalifu kuwa mpenzi wa jinsia moja, na ni nadra kushuhudiwa wachezaji wanaoweka wazi kuwa wao ni wapenzi wa jinsia moja katika soka. Lakini Phuti Lekoloane analibadili hilo. Anacheza katika daraja la tatu la soka Afrika kusini anajaribu kubadili mitazamo ya watu dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kutoa nafasi kwa wachezaji zaidi kujitokeza wazi.