Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wazazi wake wanapokezana ili kumuamsha kila baada ya dakika kadhaa
Mtoto wa miezi sita katika mji wa Delhi nchini India anakabiliwa na ugonjwa unaoathiri mfumo wa fahamu, hali ambayo inamzuia kulala usingizi mzito kwasababu anaweza kuacha kupumua. Kwahiyo wazazi wake wanapokezana ili kumuamsha kila baada ya dakika kadhaa. Wanasema anahitaji kufanyiwa upasuaji maalum ambao unagharimu zaidi ya dola 50,000 fedha ambazo ni changamoto kubwa kwao kuzipata.