Oliver Mtukudzi: Mwanamuziki nguli amefariki dunia Zimbabwe

Oliver Mtukudzi

Chanzo cha picha, C Brandon

Maelezo ya picha, Muziki wake Oliver Mtukudzi wa mtindo wa afro-jazz, ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani
Muda wa kusoma: Dakika 1

Mwanamuziki nguli kutoka nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi amefariki dunia.

Amefariki hii leo katika hospitali ya Avenues mjini Harare.

Mtukudzi amekuwa akiugua kwa muda sasa.

Alilazimika kukatiza miadi kadhaa katika fani hiyo ya muziki katika mataifa mbali mbali duniani kutokana na kuugua kwake.

Muziki wake wa mtindo wa afro-jazz ulivuka mipaka na kupata mashabiki wengi kote duniani.

Alipata umaarufu nchini Zimbabwe kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo 1980 alipojiunga katika jeshi na muimbaji mwenza wa Zimbabwe anayeishi Marekani, Thomas Mapfumo kutoa sauti ya mapinduzi katika wakati ambapo nchi hiyo ilikuwa inakabiliana na serikali ya Ian Smith.

Baada ya uhuru wa nchi hiyo, aliitumia sauti yake kuzungumzia masuala ya kisiasa na ya kijamii.

Kwa mara nyingi ujumbe ndani ya muziki wake ulikuwa ni wa ndani kukwepa mkono wa serikali iliyokuwa haipendelei kukosolewa.

Mtukudzi amekuwa katika taaluma ya muziki kwa zaidi ya miongo minne, na amefanikiwa kutoa albamu 67.

Albamu yake ya mwisho imeangazia hali ya kisiasa hivi sasa Zimbabwe na matatizo ya kijamii.

Nyota huyo wa muziki kutoka Zimbabwe alikuwa anapewa heshima ya muziki wa Afrika kama ilivyo kwa wasanii kama Hugh Masekela, Steve Dyer, Miriam Makeba, Yousssou N dour, Angelique Kidjo, Yvonne Chaka Chaka na Lady Smith Black Mambazo.

Risala zamiminika

Mara baada ya taarifa za kifo chake Mutukudzi kuchipuka, mashabiki wake wametuma risala zao katika mitandao ya kijamii

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2