Shambulio 14 Riverside Nairobi: Tulisikia boom, kama bomu

Polisi nchini Kenya wanaendelea kukambiliana na watu wenye silaha walioshambulia majengo ya 14 Riverside, mtaa wa Westlands jijini Nairobi.

Walioshuhudia wanasema walisikia milipuko miwili ikifuatiwa na mfululizo wa ufyatuaji wa risasi.

Mmoja wao amezungumza na mwandishi wa BBC Bashir Mohammed, na kueleza aliyoyaona na kuyasikia.