Njia ya kipekee ya 'kuufunga mwaka' Peru – kwa kupigana ngumi

Kabla ya Mwaka Mpya kuanza katika mkoa wa Chumbivilcas, nchini Peru, wenyeji huwa na utamaduni wa kipekee wa kuufunga mwaka kwa kupigana ngumi.

Watu hukusanyika na wale wenye mizozo hupigana ngumi na kutatua migogoro yao.

Lengo huwa ni kuhakikisha wakazi hawavuki na mizozo kwenye mwaka mpya.