Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wasentinele: Kabila hili la watu weusi linaloogopewa sana India lilitoka wapi?
Raia wa Marekani John Allen Chau aliuawa wiki iliyopita kwa kufumwa mishale na watu wa kabila la Sentinele wanaoishi katika kisiwa cha Sentinele Kaskazini.
Kabila hilo ni miongoni mwa watu wa jamii kadha ambazo zinakabiliwa na hatari ya kuangamia zinazoishi katika mkusanyiko wa visiwa vya Andaman na Nicobar vinavyomilikiwa na India.
Watu hawa ni wa aina gani? Wana uhusiano na Afrika?