Kashfa ya madawa Kenya: Je ni kweli kwamba asilimia 30 ya dawa nchini humo ni bandia?

Biashara ya dawa bandia duniani inakisiwa kufikia dola bilioni 30 kulingana na Shirika la Afya Duniani WHO.

Nchini Kenya, Muungano wa Wafamasia unakadiria kwamba asilimia 30 ya dawa nchini ni Bandia huku dawa za kupambana na malaria na antibiotic zikiathirika pakubwa.

Kitengo cha afya cha BBC Life Clinic kimeweza kuchunguza jinsi dawa duni huingizwa nchini Kenya na uwezo wa kusababisha madhara.

Ripoti: David Wafula