Watu walio na matatizo ya kiakili wanavyotendewa unyama vituo vya maombi Ghana

Mataifa yenye pato la chini hutumia kwa wastani 0.5% pekee ya bajeti katika huduma ya matatizo ya afya ya kiakili kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Nchini Ghana, hilo limechangia kuwepo kwa mtaalamu mmoja pekee wa afya ya kiakili akihudumia watu 1.2m.

Watu wengi wenye matatizo ya kiakili wamekuwa wakikimbilia “kambi za maombi” na vituo vingine vya kiroho na kitamaduni kupata tiba.

Wengi hudhalilishwa na kutendewa ukatili katika vituo hivyo.

Uchunguzi wa BBC umebaini kwamba katika kituo kimoja cha maombi, wagonjwa huzuiliwa kwenye vizimba.

Mwandishi: Sulley Lansah

Mwandaaji: Annie Duncanson

Video na uhariri wa video: Christian Parkinson