Je unajua ni kwanini harufu ya mwanamke huvutia au kumchukiza mwanamume?

Wanasayansi wamegundua ni kwanini wanaume huvutiwa au kuchukizwa na harufu za wanawake. Sampuli za harufu za makwapani za baadhi ya wanawake zilikusanywa na wanasayansi katika chuo kikuu cha Bern na wanaume kadhaa wakapewa kuzinusa na kuziorodhesha. Siri wamegundua ipo kwenye viwango vya homoni mwilini.