Nidhamu ya matumizi ya simu: Mambo matano ya kukuepusha kuwakera wengine

Mashabiki wakitumia simu zao wakati wa tamasha

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mashabiki wakitumia simu zao wakati wa tamasha
    • Author, Na Marie Jackson
    • Nafasi, BBC News
  • Muda wa kusoma: Dakika 2

Ni kitu cha kwanza wengi wetu tunakitazama asubuhi na kitu cha mwisho kukiangalia usiku.Simu zetu haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika 12, kwa mujibu wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Uingereza, Ofcom.

Ni mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo tunakudokeza sheria tano za matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini.

1.Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula

Watu wengi hufanya hivyo, na zaidi ya 26% ya vijana wanakubali suala hili

''Simu zinapaswa kuwa zimezimwa saa zote wakati wa chakula, mikutano na sherehe,''anasisitiza Diana Mather, mshauri wa masuala ya tabia.

''Mtu uliyenaye ni mtu aliye muhimu zaidi.Hakuna miongoni mwetu asiye na umuhimu.

Hata kutazama televisheni inakuwa imezimwa kwa baadhi ya watu wakati mkiwa kwenye meza ya chakula

Zaidi ya watu wanne kati ya watano walio na umri wa miaka 55 na zaidi wanafikiri haikubaliki kutazama ujumbe wa simu ukilinganisha na 46% ya umri wa miaka 18 mpaka 34.

2. Kusikiliza muziki wenye sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma

Kitaalamu huitwa sodcasting yaani tabia ya kusikiliza muziki kutoka kwenye simu au vifaa vingine kwa sauti kubwa bila kujali wanaokuzunguka.

Inahusisha kutazama video au kucheza michezo ya kwenye simu kwa sauti kubwa.

76% kati yetu tunalipinga lakini hatuachi tabia hiyo.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2

Mwisho wa X ujumbe, 2

3.Kuzungumza na simu wakati unapotakiwa kumsikiliza mtu mwingine

''Kutuma ujumbe na kuzungumza ni tabia mbaya sana,''anasema mtaalamu Diana Mather.

Ikiwa hatupeani muda sisi wenyewe, tunapoteza nafasi kubwa sana ya kufahamiana vizuri''.

Wanasiasa wenzake John McDonnell huenda walikosa kumfahamu kansela kivuli wakati wa kipindi cha bunge la commons kikiendelea

Alikuwa na cha kusema wakati wa kutoa taarifa mwaka 2016 lakini wenzake walikuwa wakitazama simu zao za mkononi.

Wabunge wakitazama simu zao
Maelezo ya picha, Wabunge wakitazama simu zao

4. Kutembea huku ukitazama simu yako

Huinamisha vichwa, macho yakiwa kwenye kioo cha simu, wanakuja upande ambao upo.Kimoyomoyo unapiga kelele tazama mbele! tazama mbele!

Mwanamke akiwa makini kwenye simu yake

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwanamke akiwa makini kwenye simu yake

Na mtumiaji wa Twitter @tiredhorizon ametoa onyo kwa Umma weka simu yako mbali unapokuwa kwenye majengo ya umma, hospitali na karibu na maeneo magari aina ya malori yanapogeuza.

Alisema amekuwa akishuhudia watu wakijigonga kwenye mbao za matangazo, au wakiwagonga wagonjwa wakiwa kwenye vitanda hospitalini.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

5. Kutazama simu yako wakati ukiwa na wengine mkitazama televisheni

Familia ikitazama televisheni wakati wakiwa na vifaa vya mawasiliano

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia ikitazama televisheni wakati wakiwa na vifaa vya mawasiliano

Kati ya watu 10, wanne (41%) ya watu wazima wanaona kuwa haikubaliki kutumia simu wakati uko na familia kwenye sofa mkitazama televisheni.