Jivunie Mbunda anazungumzia kukataliwa kwasababu ya ulemavu Tanzania
Jivunie Mbunda ni mwanamume mwenye ulemavu Tanzania. Amemuoa Bahati Ramadhani tangu Mei mwaka huu. Hatahivyo kabla ya kupata upendo na furaha hii - anakiri haikuwa rahisi kwani aliwahi kukataliwa zaidi ya mara kumi kutokana na ulemavu wake. Anazungumzia changamoto za mlemavu kukubalika katika jamii Tanzania alipokutana na mwandishi wa BBC Eagan Salla.

