Wanawake wa Afrika walioibadili dunia: Amina - Malkia shujaa aliyewaongoza wanaume vitani
Amina alikuwa Malkia Shujaa wa Hausa wa ufalme wa Zazzau, ambao sasa ni eneo la kaskazini magharibi Nigeria. Ametajwa kuwa miongoni mwa mashujaa wengi tu, anaaminika kuwa kiongozi halisi aliyeongoza jeshi la wanaume katika vita tofuati.
