Hili ni boti lililo tengenezwa kwa taka za plastiki Lamu Kenya
Kikundi kimoja cha mafundi wa kutengeneza boti katika mji wa Lamu, pwani ya Kenya kimekuwa kikiunda boti ya aina yake itakayo safiri hadi Afrika Kusini. Kile kinachovutia zaidi ni kwamba boti hiyo inatengenezwa kutokana na taka za plastiki, lengo ni kutoa ujumbe wa kukabiliana na matumizi mabaya ya plastiki.


