Uchaguzi ulivyoosababisha mauti na kilio Kenya

Uchaguzi wa marudio ulipokuwa unafanyika, katika maeneo mengi ngome za upinzani makabiliano yalishuhudiwa kati ya wafuasi wa Bw Raila Odinga na polisi.

Katika makabiliano hayo, baadhi ya watu ambao jamaa zao wanasema hawakuwa wanashiriki maandamano hayo walipigwa risasi na kuuawa.