Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Kenya: Nini kitatendeka baada ya Odinga kujiondoa?
Nchini Kenya mjadala unaendelea kufuatia kiongozi wa upinzani Raila Odinga kujiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26.
Kumekuwa na maswali mengi kuhusu je uchaguzi utafanyika au mgombea aliyebaki Rais Uhuru Kenyatta atangazwe kuwa mshindi bila kufanyika uchaguzi.
Tayari Rais Uhuru Kenyatta amesema pamoja na kujiondoa Raila Odinga wa NASA uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.
Katika kupata ufafanuzi zaidi kuhusu utata huo Mwandishi wetu Idris Situma amezungumza na Dkt Alutalala Mukhwana ambaye ni mwanasheria aliyebobea katika masuala ya Kikatiba.