Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Changamoto katika kukabili ndoa za utotoni Tanzania
Sheria ya msingi ya ndoa nchini Tanzania iliyopitishwa mwaka 1971 inataja ndoa za kulazimishwa kama ni kosa la jinai.
Tanzania hata hivyo imetajwa kuwa ni moja kati ya nchi zenye viwango vya juu vya matukio ya ndoa za utotoni, nyingi ambazo ni za kulazimishwa, katika utafiti uliochapishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) 2016.
Nchi hii inatajwa kuwa ni nchi ya tatu barani Afrika kwa matukio ya ndoa na mimba za utotoni kwa asilimia 28%.
Mwandishi wa BBC Maximiliana Mtenga ameandaa taarifa ifuatayo.