Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Polisi watumia nyimbo kukabili ajali za pikipiki Tanzania
Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini Tanzania kwa mwaka 2016 pekee kumetokea ajali za pikipiki zaidi ya 2000 na kusababisha zaidi ya vifo vya watu 600.
Katika juhudi za kudhibiti ajali hizo polisi wamekuja na mbinu mpya ambapo wanapowakamata madereva wa pikipiki wanaovunja sheria za barabarani huwaimbisha nyimbo ambazo huamini zitakaa vichwani mwao na kujirudia pindi wawapo barabarani.
Kwa kina mwandishi wa BBC Humphrey Mgonja anaeleza.