Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanamke awawezesha wanafunzi Kenya kutazama anga za juu
Somo la Sayansi huchukuliwa na wengi kama somo gumu hususan kwa wasichana.
Hata hivyo Susan Murabana kutoka Kenya ameanza mradi wa kuwafunza wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kama njia ya kuwafanya wapende somo hilo.
Kupitia kwa mradi wake wa 'Travelling Telescope', Susan amekuwa akitembelea shule mbalimbali, Afrika mashariki, kama anavyoarifu Anthony Irungu.