Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbona Watanzania wanatimuliwa Msumbiji?
Mamia ya raia wa Tanzania wanaoishi na kufanya biashara katika mji wa Montepuez nchini Msumbiji wameanza kuvuka mpaka na kurejea nchini mwao huku wengine wakikimbilia porini kuepuka vitendo vya kikatili vinavyodaiwa kufanywa na askari nchi hiyo wanaoendesha msako dhidi ya wahamiaji haramu.
Mwandishi wetu Omar Mutasa kutoka Afrika Kusini amefanya mahojiano na kaimu Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Bi Helena Kaffumba na kumuuliza kwa nini kumekuwa na hali hiyo nchini Msumbiji