Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Panya buku kutumika kupima kifua kikuu Tanzania
Tanzania imezindua maabara kubwa ya aina yake mjini Dar-Es-Salaam inayopima ugonjwa wa kifua kikuu (TB) kwa kutumia panya buku.
Kwa mujibu wa wataalamu wa maabara hiyo, panya mmoja ana uwezo wa kupima sampuli 100 na kutoa majibu ndani ya dakika 20 ikilinganishwa na njia nyingine ambapo majibu ya sampuli hutolewa kwa wastani wiki mbili. Je inawezekanaje? Hebu msikilize Regina Mziwanda.