Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mamba mkubwa Kenya ‘Big Daddy’ kufunga ndoa
Mmoja ya mamba wakubwa zaidi duniani kwa jina Big Daddy, ambaye anafugwa katika katika Mamba Village, mjini Mombasa, hatimaye atafungishwa ndoa rasmi na wake zake wawili, Salma na Sasha.
Hafla hiyo ya kipekee inatarajiwa kufanyika Aprili tarehe 29 mwakani mjini Mombasa.
Waandalizi wa ndoa hiyo wanasema wameamua kumsaidia Big Daddy afanye harusi baada ya kuwapa wake zake wawili penzi moto kwa miaka 30.
Katika Mamba Village, sehemu iliyo maarufu kwa ufugaji wa mamba, kuna zaidi ya mamba elfu kumi.
Mwandishi wa BBC John Nene alizungumza na waandalizi wa harusi hiyo.