Kwa Picha: Mfalme Akihito wa Japan

Mfalme wa Japan Akihito ameeleza mapenzi yake ya kutaka kung'atuka. Akihutubia taifa hilo kupitia runinga, amesema ana wasiwasi kwamba umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.

Mfalme Akihito akihutubu, 8 Agosti 2016

Chanzo cha picha, NHK

Maelezo ya picha, Kwenye hotuba yake ya pili kabisa kupitia runinga, Mfalme Akihito ameambia taifa hilo kuhusu changamoto za kuendelea na majukumu yake huku akitatizwa na umri na afya.
Mfalme Akihito wakati wa kutawazwa kwake eneo takatifu la Ise Grand Japan, 27 Novemba1990.

Chanzo cha picha, Kyodo

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito alitawazwa 1990, baada ya kifo cha babake, Hirohito, mwaka uliotangulia.
Akihito, na mchumba wake Michiko Shoda, ambaye baadaye alikuwa Malkia Michiko

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito alimuoa Malkia Michiko, raia wa kawaida, mwaka 1959. Walikutana wakicheza tenisi.
Mfalme Akihito

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Akihito amekumbatia maisha ya kisasa tangu aingie madarakani, na kuipeleka familia ya kifalme karibu na wananchi.
Mfalme Akihito na Malkia Elizabeth II Buckingham Palace, London on 26 Mei 1998.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kihistoria, mfalme alitazamwa kama 'miungu'. Hata hivyo, majukumu yake yalibadilishwa na kuwa 'ishara ya taifa' kwenye katiba mpya iliyoandikwa baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na nchi za Muungano baada ya Japa kushindwa vitani.
Mfalme Akihito na Malkia Michiko wapiga magoni mbele ya altari makumbusho ya waathiriwa wa vita Tokyo 15 Agosti, 2015.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito mara kwa mara ameeleza masikitiko yake kutokana na vitendo vya Japan wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, jambo lililomfanya kutofautiana na viongozi kadha waliotaka kubadilisha mwenendo wa taifa hilo.
Mfalme Akihito

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mwaka 2011, Mfalme Akihito na Malkia Michiko walisifiwa kwa kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga na tetemeko la ardhi. Mfalme Akihito pia alitoa hotuba yake ya kwanza kwa umma kupitia video.
Mfalme Akihito na Malkia Michiko wapungia mikono wananchi Hayama, karibu naTokyo. (5 Februari 2016.)

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mfalme an Malkia wamesimamia kipindi cha mabadiliko makubwa Japan na kuwa karibu zaidi na raia. Maelfu ya watu hufika kila mwaka mpya makao makuu ya kifalme kuwatakia heri.
Gazeti la Japan

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Taarifa zilizotokea Julai kwamba Mfalme Akihito huenda angeng'atuka, jambo ambalo halijawahi kufanyika Japan, zilishangaza wengi.
Mfalme Akihito

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Lakini katiba inamzuia kuingilia siasa za nchi hiyo, na kunahitajika mabadiliko kwenye sheria za nchi hiyo ili kumruhusu kung'atuka.
Mfalme Akihito akiwa kwenye treni Tokyo (25 Julai 2016)

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mfalme Akihito , ambaye ametatizwa na afya yake miaka ya karibuni, anataka kukabidhi baadhi ya majukumu kwa watu wengine wa familia yake.
Mfalme Akihito 2 Januari 2014.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Mwishowe, mrithi wake atakuwa Mwanamfalme Naruhito, anayeonekana hapa upande wake wa kulia.
Watu wamtazama Mfalme Akihito akitoa hotuba kupitia televisheni.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Kupitia hotuba ya video ya dakika 10, ambayo ilirekodiwa awali, Mfalme Akihito amesema anatumai majukumu ya mfalme kama ishara ya taifa yataendelea bila matatizo.
Mfalme Akihito 2 Januari 2016.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Akihito ndiye Mfalme wa 125 katika familia ya kifalme ambayo inaaminika kutawala tangu karne ya tano, jambo linaloifanya kuwa familia ya kifalme ya kale zaidi duniani.