Visa vya corona vya pungua kote duniani

Maelezo ya sauti, Visa vya corona vya pungua kote duniani

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kuwa maambukizi ya virusi vya corona kote duniani yamepungua kwa wiki tano mfululizo. WHO imeongeza kuwa idadi ya maambukizi mapya kwa sasa ni milioni mbili kwa wiki ikilinganishwa na mwanzoni mwa mwaka ambayo kwa wiki maambukizi mapya yalikuwa milioni tano.