Mchezaji wa kimataifa wa Kriketi Moeen Ali ameambukizwa Covid-19
Mchezaji wa kimataifa wa mchezo wa Kriketi wa England Moeen Ali ameambukizwa Covid -19 ,baada ya kufanyiwa Vipimo akiwa nchini Sri-Lanka na kikosi chake. Kwa sasa atajitenga kwa muda wa siku 10 kulingana na utaratibu wa serikali ya Sri- Lanka. England wapo Sri Lanka kushiriki mchezo wa Kriketi unaoanza Januari 14 , hivyo Moeen Ali huenda akakosa kushiriki.
