Matt Lima: Polisi awanunulia wezi chakula cha Krismasi
Afisa mmoja wa polisi nchini Marekani ambaye aliitwa kukamata familia inayoshukiwa kuiba ndani ya duka la jumla, badala yake aliwanunulia chakula ili wapate kula chakula kizuri cha Krismasi. Matt Lima alichukua uamuzi huo mwezi uliopita baada ya familia hiyo kusema wamepata wakati mgumu kifedha na walikuwa hawana chakula cha kuwalisha watoto wao. Je ,wewe umefanya ukarimu upi wakati huu mgumu wa corona? sema nasi bbcswahili.