Roboti inayowashughulikia wagonjwa wa corona Nigeria

Wanafunzi kutoka shule ya Kimataifa ya Glisten huko Abuja Nigeria,wameanzisha teknolojia inayoitwa Mairobot, kuzuia wahudumu wa afya nchini humo kuambukizwa virusi vya corona.Teknolojia hiyo inatumia roboti kushughulikia wagonjwa wa Corona. Je ? unadhani mataifa mengine yanafaa kuiga mfano huu? sema nasi BBCSwahili.