Meneja wa Arsenal asema ana matuimaini ya Arsenal bora zaidi
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anasema kuwa ni matumaini yake kuwa sare waliopata walipochuana na Southampton itadhihirisha kuwa timu yake sasa imeanza kupata mafanikio katika michuano ya Ligi kuu ya England. Arsenal walilazimika kucheza mechi hiyo na wachezaji 10 baada ya Gabriel kuonyeshwa kadi mbili za manjano kwa mda wa dakika nne.
