Mwanamuziki wa Marekani huenda akafungwa miaka 10 jela
Mwanamuziki wa Rap kutoka Marekani lil wayne huenda akapewa hukumu ya miaka 10 jela baada ya kukiri kumiliki bunduki ya dhahabu pamoja na risasi kinyume cha sheria.
Lil Wayne mwenye umri wa miaka 38 amekiri kuwa na bunduki hiyo wakati alipokuwa akisafiri kuelekea Florida kwa ndege binafsi mnamo Desemba mwaka jana.