Licha ya janga la Corona, Swift azindua albamu ya pili mwaka huu.

Maelezo ya sauti, Licha ya janga la Corona, Swift azindua albamu ya pili mwaka huu.

Taylor Swift ametoa albamu yake ya pili ya mwaka wa 2020 usiku wa manane, kama alivyoaahidi kwenye mtandao wa Twitter. Evermore inaelezewa kuwa kama "albamu dada" kwa ile ya Folklore, ambayo yenyewe pia ilizinduliwa ghafla mwezi wa Julai.Swift amesema mkusanyiko mpya wa nyimbo 17 wote umetokea kutoka kipindi hicho cha vizuizi vikali vya kutangamana.