Britney Spears anyimwa haki ya kumiliki mali yake.
Mahakama moja nchini Marekani imekataa ombi la mwanamuziki maarufu Britney Spears kutaka babake aondolewe kama mlinzi na mhifadhi wa mali yake. Jamie Spears amekuwa akihifadhi mali ya binti yake kwa miaka 12, kufuatia wasiwasi wa afya yake ya kiakili. Britney Spears amewika na kibao "Born to make you happy."