Albamu mpya ya Wizkid ya 'Made in Lagos' yafurahisha wengi.

Jina la Wizkid na lile la la albamu yake mpya, Made In Lagos, ndio linaloongoza kwenye mtandao wa Twitter nchini Nigeria tangu jana alipokuwa anazindua albamu hiyo hadi sasa. Ni albamu ya kwanza ya mwanamuziki huyo katika kipindi cha miaka mitatu, na imepokea sifa kem kem kutoka kwa wakosoaji likiwemo gazeti la Guardian la Uingereza.