Mwanamuziki maarufu atangaza kumuunga mkono Biden

Maelezo ya sauti, Mwanamuziki maarufu atangaza kumuunga mkono Biden

Mwanamuziki maarufu Jennifer Lopez na mchumba wake Alex Rodriguez wametangaza msimamo wao rasmi wa kumuunga mkono mgombea wa urais kupitia chama cha democrats Joe Biden katika uchaguzi wa Marekani mwezi ujao.Wakati wa mazungumzo ya video ya moja kwa moja wawili hao wamesema wanataka kuungana pamoja na kukabiliana na maradhi ya covid -19 pamoja na kuinua tena uchumi wa taifa la marekani kwa kumchangua kiongozi anaefaa.