Kanye ataka kukomeshwa kwa ukatili wa polisi nchini Nigeria
Rapa wa Marekani Kanye West ameelezea kuunga mkono raia Wanigeria ambao wanapinga ukatili wa polisi unaofanywa na Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi (Sars). Maandamano yaliyoenea nchini humo yamemlazimu Rais Muhammadu Buhari kuvunja kitengo hicho lakini raia wanataka maafisa wa kitengo hicho kkuchukuliwa hatua zaidi.
